Matthew 15

Mapokeo Ya Wazee

(Marko 7:1-13)

1 aNdipo baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamjia Isa kutoka Yerusalemu na kumuuliza, 2 b“Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!”

3Isa akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 4 cKwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 5 dLakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’ 6basi hana tena sababu ya kumheshimu baba yake nacho. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. 7 eNinyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba:
8 f“ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao,
lakini mioyo yao iko mbali nami.

9 gHuniabudu bure;
nayo mafundisho yao
ni maagizo ya wanadamu tu.’ ”

Vitu Vitiavyo Unajisi

(Marko 7:14-23)

10 hIsa akaita ule umati wa watu, akawaambia, “Sikilizeni na mwelewe: 11 ikinachomfanya mtu kuwa najisi mbele za Mungu si kile kiingiacho kinywani mwake, bali ni kile kitokacho kinywani mwake.”

12Kisha wanafunzi wake wakamjia na kumuuliza, “Je, unajua kwamba Mafarisayo walichukizwa sana waliposikia yale uliyosema?”

13 jAkawajibu, “Kila pando ambalo Baba yangu wa mbinguni hakulipanda, litang’olewa. 14 kWaacheni; wao ni viongozi vipofu, wanaoongoza vipofu. Kama kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, wote wawili watatumbukia shimoni.”

15 lPetro akasema, “Tueleze maana ya huu mfano.”

16 mIsa akawauliza, “Je, bado ninyi hamfahamu? 17 nJe, hamwelewi kwamba chochote kiingiacho kinywani huenda tumboni, na hatimaye hutolewa nje kikiwa uchafu? 18 oLakini kitokacho kinywani hutoka moyoni, na hiki ndicho kimtiacho mtu unajisi. 19 pKwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio. 20 qHaya ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula bila kunawa mikono hakumtii mtu unajisi.”

Imani Ya Mwanamke Mkanaani

(Marko 7:24-30)

21 rIsa aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. 22 sMwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, “Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana.”

23Lakini Isa hakumjibu neno. Hivyo wanafunzi wake wakamwendea na kumsihi sana, wakisema, “Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele.”

24 tIsa akajibu, “Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea.”

25 uLakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Isa, akasema, “Bwana, nisaidie!”

26Isa akajibu, “Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

27Yule mwanamke akajibu, “Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwenye meza za bwana zao.”

28 vNdipo Isa akamwambia, “Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka.” Naye binti yake akapona tangu saa ile.

Isa Aponya Watu Wengi

29Isa akaondoka na kwenda kando ya Bahari ya Galilaya. Kisha akapanda mlimani, akaketi huko. 30 wUmati mkubwa wa watu ukamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya. 31 xHao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Isa Alisha Watu Elfu Nne

(Marko 8:1-10)

32 yKisha Isa akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu, na hawana chakula chochote. Nami sipendi kuwaaga wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani.”

33Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha umati huu wa watu mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?”

34Isa akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?”

Wakamjibu, “Tunayo mikate saba na visamaki vichache.”

35Isa akawaambia ule umati wa watu waketi chini. 36 zKisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akiisha kumshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa ule umati wa watu. 37 aaWote wakala na kushiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. 38Idadi ya watu walikuwa wanaume 4,000, bila kuhesabu wanawake na watoto. 39Baada ya kuaga ule umati wa watu, Isa aliingia katika mashua, akaenda sehemu za Magadani.
Magadani ni Magdala, mji wa Galilaya, kama kilomita 16 kusini mwa Kapernaumu.
Copyright information for SwhKC